September 27, 2013



 
KALI WAKATI AKIICHEZEA AZAM...
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amesema wamejiandaa vya kutosha kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wao Tanzania Prisons.


Azam wanatarajiwa kuvaana na Prisons keshokutwa Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara mechi itakayochezwa kwenye Uwanja Sokoine Mkoani Mbeya.

Kocha huyo alisema kuwa kikosi kipo fiti kwa ajili ya mechi hiyo, hivyo mashabiki watarajie kupata matokeo mazuri.

“Wachezaji wote wana afya njema na wapo tayari kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wetu, hivyo mashabiki watarajie kupata matokeo mazuri kutokana na maandalizi tuliyofanya,” alisema Ongala.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic