Ngedere mmoja ameamua kufanya urafiki na
beki wa Simba, Rashid Ismail maarufu kama Baba Ubaya.
Ngedere huyo sasa amebadikwa jina la
Sharobaro kutoka kwa wachezaji wa Simba walio katika kambi ya Bamba Beach, Kigamboni
nje kidogo ya jiji la Dar.
Wachezaji wa Simba wamekuwa na urafiki
mkubwa na ngedere huyo lakini yeye zaidi anavutiwa na Baba Ubaya.
Baba Ubaya ambaye amejiunga na Simba
msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ndiye amekuwa akishinda anacheza na Sharobaro.
Sharobaro naye hawezi kupitisha siku
bila ya kupiga hodi kwa Baba Ubaya na kutaka wacheze angalau kidogo tu.
“Ni rafiki yangu, kila siku lazima aje
na moja kwa moja anakuja kwangu kama unavyoona. Kila mtu hapa kambini anajua
Sharobaro ni rafiki yangu,” alisema Baba Ubaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment