Kwa mara ya pili mfululizo ndani ya wiki moja, Yanga imeambulia sare ya pili mjini Mbeya.
Yanga ikiwa mgeni wa Prisons ya Mbeya imetoka sare ya mabao 1-1.
Jumatano ilyopita, ilipata sare nyingine kama hiyo dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja huo huo wa Sokoine.
Yanga ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Jerry Tegete lakini maafande wa Prisons wakasawazisha.
Maana yake, Yanga imepoteza pointi nne katika mechi zake mbili za mjini Mbeya.
Hali inayowalazimu kubadili mwendo kwa kuwa watani wake Simba wamekuwa wakisonga mbele kwa kasi.
0 COMMENTS:
Post a Comment