Uongozi wa timu ya Tanzania Prisons umetoa neno kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ kuwa hatakiwi kuitenga timu hiyo na kuelekeza nguvu zake kwenye
kikosi cha Mbeya City pekee wakati zote ni timu za Mkoa wa Mbeya.
Katibu Mkuu
wa Prisons, Sadiki Jumbe amesema kumekuwa na hali ya upendeleo kwa wenzao wa
Mbeya City wakati huu ambapo Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea.
“Timu
zote zipo katika jimbo lake na wote ni wapiga kura wake, hivyo tunamuomba
mbunge wetu asitubague kama wananchi wanavyotutenga kwani kuna utofauti mkubwa
sana kwa sapoti wanayopewa wenzetu wa Mbeya City na sisi.
“Nilidhani
yeye ndiye angekuwa mstari wa mbele au kuwa mfano wa kutupa sapoti lakini (Sugu)
anakuwa wa kwanza kutubagua, hii hali inatuumiza sana na inawaathiri hadi
wachezaji wetu.
“Mfano mapato
ya Mbeya City na Yanga yalikuwa milioni mia lakini sisi na Yanga ni milioni arobaini
na nne, kwa nini inakuwa hivyo, inauma sana,” alisema katibu huyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment