Shabiki wa Yanga, Nehemia
Bakary alijikuta aking’atwa na mbwa wa polisi waliokuwa wakilinda getini katika
mechi ya Prisons dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Sokoine, juzi mkoani hapa.
Bakary ameliambia gazeti
hili kuwa aling’atwa na mbwa huyo wakati alipokuwa mlangoni akitaka kuingia
ambapo ghafla alirukiwa na mbwa huyo na kumng’ata mkononi.
“Mpaka askari wanaanza
kudhibiti tayari alikuwa ameshaniumiza, nilipowauliza askari wale juu ya
matibabu wakaniambia niende hospitali nikajitibu mwenyewe.
“Nashukuru nilipoingi
ndani (uwanjani) ndipo daktari wa Yanga, (Nassor) Matuzya alinipa huduma ya
kwanza wakati hasari wote waliamua kunipotezea,” alisema shabiki huyo aliyetoka
Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa sare ya
1-1.
Alipoulizwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (Mrefa), Haroub
Seleman alisema haNa taarifa zozote juu ya tukio hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment