Shabiki anayeaminika ni wa Liverpool, amemporomoshea matusi na
vitisho nahodha wa timu hiyo, Steven Gerrard huku akimtishia kuwaua mke na
watoto wake.
Balaa hilo limemtokea Gerrard wakati akiwa katika mazoezi ya timu
hiyo leo kwenye viwanja vya Melwood.
Shabiki huyo aliyekuwa upande wa uwanja huo alianza kumporomoshea
Gerrard vitisho hivyo wakati akiwa katika mazoezi ya kupiga faulo na mchezaji
mwenzake Philippe Coutinho.
Kocha Msaidizi wa Liverpool, Colin Pascoe ndiye alimpoza Gerrard
ambaye alikuwa tayari kumvaa shabiki huyo.
Baadaye mtunza vifaa, Lee Radcliffe alikwenda kumkimbiza mtu huyo
ambaye alipanda baiskeli na kuondoka eneo hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment