November 11, 2020


 IMEELEZWA kuwa aliyekuwa Mtedaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay kwa tuhuma za kuihujumu Simba.

Habari zimeeleza kuwa anahojiwa kuhusu ishu ya kudaiwa kuihujumu timu yake ya zamani ili ipate matokeo mabovu kwenye mechi za ligi zilizopita.

Mbatha anadaiwa kufanya hivyo kwa kushirikiana na Hashim Mbaga, aliyekuwa mkurugenzi wa mashabiki na wanachama wa Simba ambaye naye alifutwa kazi.


Kwa sasa Mbatha ni mshauri mkuu ndani ya Klabu ya Yanga kwenye mchakato wa kuelekea mabadiliko ambapo aliibukia huko muda mfupi baada ya kubwaga manyanga ndani ya Simba.


Chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck, Simba ilipokea vichapo kwenye mechi mbili mfululizo na kuyeyusha pointi sita ambapo ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons ilipopoteza kwa kufungwa bao 1-0 kisha ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Kutokana na matokeo hayo mabovu Simba ilifanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwa kumuondoa Mohamed Mwarami aliyekuwa kocha wa makipa pamoja na Patrick Rweyemamu ambaye alikuwa ni Meneja wa Simba.



19 COMMENTS:

  1. Msipoteze time kwa hao wajinga achaneni nao wekeni viongozi wazuri wenye mapenzi na timu

    ReplyDelete
  2. Kama alijihusisha kwenye haya mambo alitakiwa ajifunze kwanza mbinu kutoka kwa waliomtuma, ona sasa msala unaelekea kumwelemea ili hali wahusika wakuu wako pembeni. Hata ishu za kuhonga marefa na wachezaji zitajitokeza tuu

    ReplyDelete
  3. Mwandishi nae wale wale, senzo anashikiliwa kwa tuhuma za kuhujumu na kutoa rushwa sio kisa matokeo mabovu ya simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameandika kujitetea alitakiwa aeleze ameshikili kwa tuhuma za kuhujumu Simba

      Delete
  4. Hahaha mpira umeishawashinda tayari mikia mmeanza kutafuta huruma za vyombo vya Dora mlipofungwa na jkt ruvu ilikuwaje? Mwaka huu imekula kwenu kundaki nyooooooo

    ReplyDelete
  5. Huu ni upuuzi wa kiwango cha mwendo kasi.Sasa masuala ya kufirikika ya hujuma yanaihusisha vipi polisi?Seali linakuja kama watamshtaki je watamshtaki kwa kosa gani?la uhujumu uchumi au utakatishaji fedha au vipi?Je TFF wapo wapi hadi polisi wahusike? Na kama ni hujuma je waliripoti TAKUKURU? ambao kimsingi ndio wenye wajibu wa kuchunguza/kupeleleza.Polisi watuambie walizifanyiaje tuhuma za viongozi wa Simba kutaka kumhonga Ramadhan Kabwili na baadhi ya wachezaji wa Yanga,mbona hatukuwasikia polisi kuwaita viongozi wa Simba na kuwahoji ila kilichofanyika ni kwa baadhi ya viongozi hasa Hans Pope kutoa vitisho hadharani.Acheni mpira uchezwe hadharani na wala sio kutumia vyombo vya dola na nafasi za viongozi waandamizi wa serikali ambao ni mashabiki au wanachama wa Simba kunyanyasa wengine ili mradi tu mfanikishe mambo yenu.Polisi ituambie kwanza imezifanyiaje tuhuma zilizotolewa hadharani za viongozi wa Simba kuhujumu timu pinzani miezi kadhaa nyuma wakati wakiendelea kumuhoji Senzo vinginevyo nao watakuwa hawana tofauti na NEC

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo mbona mmepaniki tuhuma zenu nyingi ni za uzushi ndio maana hata Morison alipowashitaki kwa kugushi tff walikwepesha mtu aliyekuwa akiwasiliana naye yuko ndani zaidi ya wiki mbili na hizi zote ni tuhuma ikithibitika watapelekwa mahakamani Simba ni brand kubwa huwezi kulinganisha na Utopolo

      Delete
    2. Kwani umeambiwa nani kuwa issue ya Kabwili imeisha?Si aliambiwa Kabwili apeleke ushahidi na vithibitisho na hajapeleka.Hadi Leo Simba bado wanataka uthibitisho ni kiongozi gani wa Simba alitaka kumuhonga Kabwili?Hajaleta ushahidi na hajamtaja

      Delete
  6. Najiuliza swali je na wachezaji ambao inasemekana walikuwa wanatumika nao wataitwa polisi kuhojiwa maana inasemekana kuna wachezaji kadhaa ambao bado wanamkubali Senzo na wanawasiliana naye kila siku,au ndo zile shutuma za Hans Pope kwa baadhi ya wachezaji zinahusiana na kinachoendelea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unamuuliza nani?...Nenda kawaulize pale osterbay police.

      Delete
    2. We shoga umesoma vizuri na kuelewa maoni ya mchangiaji hapo juu?amesema anajiuliza swali na wala hajamuuliza mtu,acha kufikiri kwa kutumia makalio

      Delete
  7. Kama kuna wachezaji wanawasiliana nae kiurafiki hilo halina shida. Tatizo kama wanawasiliana kwa nia ya kupokea rushwa wahujumu simba, hao wataitwa. Kumbuka rushwa sio lazima upewe hela, hata kukubali kushawishiwa utende kosa nalo ni rushwa

    ReplyDelete
  8. SIMBA au mikia fc wanatapatapa tu kwahiyo wanataka Mazingisa ndo acheze hahaha mfa maji hakosi kutapa tapa

    ReplyDelete
  9. Simba Unamjuwa vizuri sio Maskini na hamu uwezo hata kidogo na bao la peneti mliozawadiwa linakusuteni na hayo munayajuwa vizuri

    ReplyDelete
  10. Polisi fanyeni kazi yenu ipasavyo, upumbavu ktk soka hautakiwi. Ndo maana MO alimtimua. Sasa anataka aonekane Bora kwanjia za panga kuwapa utopolo ubingwa wkt mwanamke Barbara ashamshinda kwamuda mfupi tu. Akikutana na kosà atimuliwe aende kwao na hao utopolo wanasajili utumbo kila siku. Emmy aliwatukana kihalali hawana akili utopolo wanasajili upumbavu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic