Timu ya AS Cannes imeporomoka kutoka
nafasi ya pili hadi ya tatu msimamo wa Ligi daraja la nne nchini Ufaransa.
AS Cannes ndiyo timu anayochezea
Mtanzania, Shomari Kapombe ambaye hata hivyo amekuwa nje kwa kipindi kirefu
baada ya kufanyiwa upasuaji kidoleni.
AS Cannes imeporomoka lakini bado ina
nafasi ya kukaa kileleni iwapo itashinda mechi yake ya Jumamosi dhidi ya vinara
wa ligi hiyo Monaco 2. Awali ilianza ligi kwa kuwa kinara, halafu ikaporomoka
hadi nafasi ya pili.
Monaco 2 iko kileleni na ponti 17 wakati
AS Cannes iko katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14, nafasi ya pili
inashikwa na Grenoble Foot 38 yenye 15.
AS cannes ilisogea hadi nafasi ya tatu
baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mont de Marsan katika mechi iliyopigwa
kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Kapombe amejiunga na timu hiyo akitokea
Simba baada ya kufuzu majaribio aliyopelekwa na wakala Mtanzania anayeishi
nchini Uholanzi, Denis Kadito.
Lakini bado hajaanza kuonyesha cheche
zake kwani siku chache baada ya kujiunga alifanyiwa upasuaji huo wa kidole.
0 COMMENTS:
Post a Comment