October 1, 2013





Kocha Jose Mourinho amekasirika na kuondoka kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliokuwa unahusu mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Chelsea itaivaa Steaua Bucharest ya Romania ambayo ni mwenyeji leo na waandishi walionekana kutilia mkazo suala la beki Kevin de Bruyne raia wa Ubeligiji ambaye Mourinho amemuacha.

Kutokana na maswali kuendelea mfululizo, Mourinho alijibu huku akionekana ana jazba na baada ya hapo akainuna na kuondoka zake akimuacha Frank Lampard amalize mkutano huo na waandishi.

"Safi sana, maana hakuna hata mmoja wenu ameuliza kuhusiana na Mara, maana kwa wiki tatu mmekuwa mkimzungumzia yeye tu.  Leo mmehamia kwa Kevin, sasa nataka kuwaambia hivi huu ni uamuzi wangu.

“Ni wachezaji11 tu wanaocheza na kocha ndiye anajua ni kina nani wanamfaa kwa wakati gani, muulizeni huyo (huku akionyesha mkono kwa Lampard), amefanya kazi nami kwa tisa, mimi si malaika, wakati mwingine ninakosea lakini ninajitahidi kuwa mkweli, hilo ndiyo muhimu zaidi.
“Sikufurahishwa na kiwango alichoonyesha Kevin katika mechi dhidi ya Swindon, baada ya hapo ameendelea kutojituma mazoezini. Sasa sioni kitu cha ajabu yeye kukaa nje,” alisema Mourinho, akainuka zake na kuondoka eneo la tukio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic