Mshambuliaji nyota wa PSG, Zlatan Ibrahimovic amefunga sehemu ya maisha yake na kueleza namna anavyovutiwa na kocha Jose Mourinho na kumponda Pep Guardiola kwamba si mtu poa.
Ibrahimovic ambaye amefanya kazi na makocha wote wawili kwa nyakati tofauti, amesema Mourinho ni kocha wa aina yake ambaye anaweza kumfanya mchezaji yoyote kuwa bora.
“Wakati mwingine alikutana na mpenzi wake na kumueleza aendelee kunifanya niwe na furaha kwa kuwa ni kiongozi wa jeshi lake. Mourinho angeweza kufanya hivyo kwa kila mtu.
“Alitaka wachezaji wake kufanya vizuri na aliwajali kwa kuwa siku zote alituita ni wanajeshi wake lakini si Guardiola,” alisema Ibrahimovic.
Ibrahimovic amesema maneno hayo katika kitabu kinachoelezea maisha yake na amefikia hatua ya kueleza hivi; kwamba Guardiola alikuwa akijaribu kuishi kama Mourinho.
“Katika michuano ya Ulaya mwaka 2008, nilipoambiwa Mourinho alikuwa anakuja kuifundisha Inter, siku iliyofuata tu akanipigia simu, nikashtuka kwa kuwa sikujua kuna nini kinaendelea.
“Alichosema ni kunieleza kwambaa nakuja kufanya kazi nasi na atafurahi tukiwa pamoja, tena alizungumza kwa Kiitaliano tena kizuri kuliko nilichokuwa nazungumza.
“Nilielezwa alijifunza kwa wiki tatu tu baada ya kujua anakuja kufanya kazi na klabu ya Italia.
“Wakati mwingine nikiwa na kikosi cha Sweden tunajiandaa na mechi dhidi ya Hispania, Mourinho alinitumia ujumbe na kunipa ushauri namna ya kufanya. Niliona anajali kama kocha wa timu ninayochezea lakini alitaka nifanye vizuri nikiwa na timu yangu ya taifa. Kabla sikuwa nimewahi kutumiwa ujumbe na kocha.
“Kuanzia hapo nilianza kuvutiwa naye sana, ni mtu anayejali, anajiamini na asiyehofia kufanya anachoamini ni sahihi kwake. Mourinho anapumua mpira kwa saa 24 za wiki.
“Lakini kama mnakutana na timu Fulani, basi hakuna kocha anayeweza kuizungumzia timu pinzani kwa uhakika, haki kipa wa tatu kama Mourinho, anajua kinachofuatia mbele yake na afanye nini.”
Ibrahimovic ambaye alifanya kazi na Mourinho akiwa Inter na baadaye Guardiola akiwa naye Barcelona, anasema Guardiola ni kocha tofauti na mwenye roho mbaya.
Anamuelezea kuwa ndiye aliyelazimisha aondoke Barca mwaka 2011 na kurudi na kujiunga na AC Milan badala ya Man City ambayo ilitaka kumpa fedha nyingi.
WENGER:
Pamoja na makocha hao wawili, Ibrahimovic ameelezea alivyokwenda kufanya majaribio Arsenal lakini baadaye akagoma kufanya.
“Nilikwenda kwenye mazoezi ya Arsenal katika eneo la St Albans, niliwaona Patrick Vieira, Thierry Henry na Dennis Bergkamp wakiwa nje ya uwanja ingawa kitu kizuri zaidi kwangu nilikuwa nakwenda kumuona Arsene Wenger. Nilijiona kama kijana mdogo na nilitamani kumuona.
“Nilikuwa natetemeka kumuona, lakini nilijisikia kutokuwa na furaha namna alivyokutana na mimi, alionyesha kunikagua sana na baadaye kutojali ingawa kweli alikuwa kati ya makocha bora duniani.
“Nilijitahidi kuwa mkimya lakini baadaye nikapoteza uvumilivu, maana alionekana kama anataka kufanya kila kitu kwa wakati mmoja na kutojali sana mimi niliyekuwa naye pale ofisini, mara aangalie dirishani mara vile.
“Alisema maneno ambayo kwangu niliona kama dharau, nilijisikia vibaya. Lakini nikamuambia anipe viatu na mara moja ningefanya majaribio lakini mwisho Hasse Borg (mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Malmo niliyokuwa nachezea wakati huo)akaingilia na kunitaka niwe kimya na kwamba baadaye nitapewa taarifa kuhusiana na hilo kama nitafanya majaribio au la.
“Baada ya hapo sikuweza kujizuia na nilisisitiza kwamba nisingefanya majaribiona Borg alimueleza hilo na huo ndiyo ukawa mwisho wa mimi kutaka kucheza Arsenal.”
0 COMMENTS:
Post a Comment