Kaimu meneja wa zamani wa Yanga, Ayoub Nyenzi alizimia
mara baada ya kugundua kuwa alikuwa ameshinda ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF
katika mikoa ya Mbeya na Iringa.
Nyenzi alizimia baada ya kuamua kuhesabu kura zake
mwenyewe na kugundua alikuwa ameshinda.
Mara tu baada ya kugundua ameshinda, Nyenzi
aliangusha kilio cha nguvu kama mtu aliyepoteza nafasi hiyo.
Baadhi ya waliokuwa katika chumba hicho cha mikutano
cha Ukumbi wa Water Front walionekana kutoelewa wakidhani amepoteza.
Lakini walielelezwa alikuwa akilia kutokana na
kugundua kwamba ameshinda na hakuchukua muda kabla ya kuanguka na kuzimia.
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya ambaye alikuwa kati
ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo, alitoa huduma ya kwanza kwa Nyenzi aliyekuwa
hajitambui kabisa.
Hata baada ya kupata fahamu, bado Nyenzi alionekana
haamini kilichotokea na kuendelea kumwaga chozi huku akiangusha kilio cha
furaha.
0 COMMENTS:
Post a Comment