Baada ya kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam FC jana, Simba inarudi uwanjani keshokutwa Alhamisi katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar ngoma itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo
itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu
katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo
Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na
Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar
es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi
moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa
kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu
vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting,
Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza
na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment