Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
umemteua Said Hamad El Maamry kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo kazi
yake kubwa ni kusimamia mali za shirikisho.
El Maamry ambaye kitaaluma ni mwanasheria na Mwenyekiti wa zamani
wa TFF wakati huo ikiwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) ataongoza bodi
hiyo yenye jumla ya wajumbe watano.
Wajumbe wengine wa bodi hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel
Bendera ambaye anakuwa Makamu Mwenyekiti, Dk. Ramadhan Dau, Mohamed Abdulaziz
na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Mashishanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment