Beki wa kushoto wa Yanga, David Luhende
ameondolewa kwenye kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Bara kutokana na kupata
majeraha ya misuli. Atakaa nje kwa wiki moja.
Luhende alipata majeraha hayo katika dakika
ya 75 kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-0.
Daktari Mkuu wa Yanga, Nassoro Matuzya alisema: “Luhende nimemuondoa kabisa kwenye kikosi kitakachoivaa Mgambo Shooting, Jumanne ya wiki ijayo baada ya kupata majeraha ya misuli, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja.”
0 COMMENTS:
Post a Comment