YUSUPH (ANAYEZUNGUMZA) AKIFAFANUA JAMBO KWA SALEHJEMBE (MWENYE MIWANI) MBELE YA WAANDISHI WENGINE WAKATI WA WAANDISHI NA WAHARIRI WALIPOTEMBELEA AZAM TV. |
Bosi mkubwa kabisa wa Azam TV, Yusuph Bakhresa ndiye alitoa wazo la kuanzishwa kwa
runinga hiyo ingawa kulikuwa na ugumu kabla wazo lake halijakubalika.
Stori ya
namna Azam TV zinaeleza, baada ya Yusuph ambaye ni wakala wa kuuza wa wachezaji
anayetambuliwa na Fifa kutoa wazo hilo, alipata upinzani mkubwa.
Hata hivyo,
baadaye wazo lake lilikubalika na tayari Azam Tv imechukua umaarufu mkubwa huku
kijana huyo akipongezwa kutokana na kuwa na wazo litakaloifanya Tanzania
kuongeza ushindani katika tasnia ya habari.
Mbali na
hivyo, vijana wengi watapata ajira na mwenye amesema anaamini baada ya muda
Azam TV itakuwa maarufu nje ya Tanzania.
“Ni kweli,
nilianzisha wazo hilo, baadaye nikaenda kujifunza mambo. Familia ilinipa sapoti
lakini kama ilivyo kawaida kama linatokea jambo lazima kuna mjadala.
“Lakini
walinielewa na mambo sasa yameanza kwenda, ila tulichopanga ni kufanya mambo
kitaalamu zaidi ndiyo maana unaona mitambo tunayonunua ni ghali na ya kisasa
zaidi,” alisema Yusuph.
Azam Tv ndiyo
yenye haki ya kuonyesha Ligi Kuu Bara moja kwa moja na tayari imetoa mamilioni
ya fedha kwa timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo.
Matangazo
yake yameanza kuruka lakini kupitia TBC1 na msisitizo wa Azam TV bado
wanajipanga hadi watakapopata kiwango bora wanachokitaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment