Kiungo
nyota wa Barcelona, Cesc Fabregas amewataka mashabiki wa timu yake kuondoa hofu
ya namna ya kuwazuia wachezaji wawili wa Real Madrid.
Cristiano
Ronaldo na Gareth Bale ndiyo gumzo, kwamba Barcelona watawazuia vipi.
Lakini
Cesc amesema si kazi ngumu nay a kutisha badala yake inawezekana huku
akikumbushia wakati akicheza Arsenal.
Picha
kadhaa zinaonyesha akipambana na Bale wakati akiwa Tottenham, hali inayomfanya
asiwe na hofu hata kidogo kuhusiana naye.
Kwa
upande wa Barcelona, Lionel Messi na Neymar ndiyo wanaonekana watakuwa tatizo
kubwa kwa Real Madrid.
Hata
hivyo, mechi hiyo itakayopigwa leo saa moja usiku inatarajiwa kuwa na burudani
kali zaidi kwa kuwa kila timu ina wachezaji wengi ‘noumaa’.
0 COMMENTS:
Post a Comment