Mechi ya leo Jumamosi ya La Liga
kati ya Barcelona dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid itashuhudiwa na
mashabiki wapatao milioni 400 kupitia runinga.
Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Cam Nou
jijini Barcelona, Hispania itashuhudiwa na idadi hiyo ya mashabiki wa soka kote
duniani, wakiwemo wa Tanzania.
Waandishi 705 kutoka katika vyombo mbalimbali 146 vya habari, kutoka katika nchi tofauti 30
duniani, wameomba kuripoti mechi hiyo ‘live’.
Katika vyombo hivyo vya habari 146 vilivyoomba
vitambulisho kwa ajili ya kurupoti, waandishi 73 wanatokea katika magazeti, 33 kutoka katika runinga mbalimbali na 22 mawakala maalum wa masuala
ya habari wakati redio ni watu 18 tu.
Tayari imeshaelezwa kuwa mchezo huo
pia utaonyeshwa kutumia mifumo ya kisasa ya runinga ya high definition (HD) na 3D
kupitia Mediapro.
Hata hivyo, taarifa nyingine
zimeelezwa, mechi hiyo maarufu zaidi ya watani wa jadi duniani itaonyeshwa
dunia nzima kasoro katika bara la Oceania.
0 COMMENTS:
Post a Comment