Kipa wa zamani wa Simba, Juma Kaseja, amempigia simu
kipa namna moja wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ na kumuambia maneno kadhaa ya
kiutu uzima.
Kaseja ambaye aliachwa Simba kwa kisingizio cha
kuporomoka kwa kiwango chake, amempigia simu Barthez na kumueleza kwamba
anatakiwa kuwa mvumilivu sana katika suala la mpira wa Tanzania.
Barthez alikuwa kipa mbadala wa Kaseja wakati wote
wakiwa Simba, kabla ya yeye kuhamia Yanga ambako amefanikiwa kuwa kipa namba
moja.
Chanzo cha uhakika kimeeleza, Kaseja aliamua kufanya
hivyo baada ya kuona matatizo yaliyomkuta Barthez ya kuangushiwa mzigo, kwamba
ndiye aliyesababisha Simba kusawazisha mabao yote matatu na mechi kati ya timu
hizo kumalizika kwa sare ya mabao 3-3.
“Kaseja alikwenda (uwanja wa) Taifa siku ile, tangu
pale alionyesha kuumizwa sana na Barthez kuangushiwa mzigo. Siku iliyofuata
alimpigia simu na kumueleza kwamba anapaswa kuwa mvumilivu sana kwa kuwa mpira
ndiyo kazi yake.
“Barthez alionyesha kufarijika na alimueleza Kaseja
anavyoumia hasa kuhusiana na mabao yalivyotokea na mashabiki wasiokuwa makini
wanavyomtwisha mzigo. Lakini inaonekana maneno hayo ya Kaseja, yamemsaidia
sana,” kilieleza chanzo hicho.
Hivi karibuni, mashabiki wa Yanga walivamia nyumbani
kwa Barthez eneo la Chanika jijini Dar es Salaam wakitaka kumpiga kwa madai
ndiye aliyechangia Simba kusawazisha mabao matatu katika mechi hiyo ya Ligi Kuu
Bara iliyochezwa Jumapili iliyopita.
Hata hivyo, wengi wenye utaalamu wa mpira wamekuwa
wakikosoa tofauti na kueleza mabao hayo yalitokana na uzembe wa safu ya ulinzi
na hasa mabeki.
Tayari kocha, Ernie Brandts ameshampumzisha Barthez
katika mechi ya Yanga dhidi ya Rhino juzi na Deogratius Munish ‘Dida’ akapewa
nafasi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment