Kocha wa Yanga, Ernie
Brandts ametamka kwamba mpaka sasa hajui nini kilichotokea katika kipindi cha
pili, wakati Yanga ikitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Simba, lakini akawashukia
mastaa katika kikosi hicho.
Brandts amesema
ameshindwa kugundua kilichosababisha sare hiyo mpaka sasa, ambapo amewataka
nyota katika kikosi hicho kutambua kuwa hakuna mtu mwenye nafasi ya kudumu
ndani ya timu hiyo.
Brandts amesema katika
mchezo uliopita dhidi ya Rhino Rangers ambao Yanga ilishinda kwa mabao 3-0,
alikibadilisha kikosi hicho na kuwaweka nje baadhi ya wachezaji mastaa, ambapo
amewataka wote katika timu yake kutambua kuwa timu yake ina jumla ya wachezaji
28 wenye uwezo mkubwa.
“Najiuliza kila mara nini
kilitokea katika mchezo wetu dhidi ya Simba, nakosa jibu sahihi, lakini ndiyo
soka, nimewaambia wachezaji wangu kuanzia mchezo wa jana (juzi), hakuna mtu
mwenye namba ya kudumu, kila mtu ana haki sawa,” alisema Brandts.
“Nitampa nafasi mchezaji
yeyote atakayekuwa sawa kwa asilimia mia moja, wachezaji wote wanatakiwa
kutambua kuwa, timu yangu ina wachezaji 28, hakuna anayemzidi mwenzake kwa
umuhimu.
“Sitaki kubadili kikosi
mara kwa mara, lakini nitafanya hivyo kama nikigundua kuwa kuna wachezaji
wameridhika na mafanikio ya muda mfupi,” alisisitiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment