Inawezekana kabisa kiungo
mkongwe zaidi wa Manchester United, Ryan Giggs ataweka rekodi itakayokaa muda
mrefu zaidi katika ligi hiyo.
Hadi sasa anaongoza kwa
kucheza mechi 620 za Premiership, anayemfuatia ni kipa wa zamani wa Liverpool
na Portsmouth, David James, mwenye 572.
Frank Lampard wa Chelsea
ana mechi 552 na ndiye pekee anayeweza kufikia rekodi ya Giggs kwa kuwa bado
anaendelea kucheza katika ligi hiyo ingawa inaonyesha anahitajika kudumu kwa
zaidi ya misimu mingine minne.
Katika idadi ya wachezaji
wenye mechi nyingi, ndani ya 10 bora ni Giggs na Lampard tu ndiyo wanaoendelea
kucheza hadi leo.
Maana yake kufikia rekodi
ya mkongwe huyo haiwezi kuwa kazi rahisi. Giggs ana miaka 39 na alianza kucheza
ligi hiyo kwa mara ya kwanza katika msimu wa 1990-91.
10 BORA YA WALIOCHEZA
MECHI NYINGI:
1 Ryan Giggs 620
2 David James 572
3 Frank Lampard 552
4 Gary Speed 534
5 Emile Heskey 517
6 Jamie Carragher 508
7 Phil Neville 505
8 Mark Schwarzer 504
9 Sol Campbell 503
10 Gareth Barry 500
0 COMMENTS:
Post a Comment