KOCHA WA SIMBA, ABDALLAH KIBADENI AKITOA NASAHA KWA WACHEZAJI WAKE WAKATI WA MAPUMZIKO DHIDI YA COASTAL UNION, WALISHINDWA KUINGIA VYUMBANI KUTOKANA UCHAFU. |
Unaweza
kudhani ni miujiza, lakini ndiyo hali halisi na huenda mambo huwa magumu zaidi
zinapokwenda timu ambazo hazina majina makubwa kucheza kwenye Uwanja wa
Mkwakwani mjini Tanga.
Uwanja
ni mchafu umepitiliza, hasa katika suala la vyoo na vyumba vya kubadilishia
nguo.
Simba
walilazimika kukaa nje wakati wa mapumziko wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara
iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana, Jumatano.
Unaweza
kusema Simba walihofia ushirikina, lakini ukibahatika kuingia kwenye vyumba au
vyoo, ni hatari na vigumu kama kuamini uwanja huo upo katika karne tunayoishi.
Swali,
vipi mechi zinachezwa, uwanja unaingiza fedha na hakuna marekebisho yoyote
yanayofanyika.
Lakini
timu za Tanga ambazo ni Coastal Union na Mgambo Shooting, vipi wanaliona suala
hilo ni kama la kawaida tu.
Kuna
sababu ya kufanya mabadiliko, au uwanja huo ukubali ukatwe fedha kila mechi na
zitumike kutengeneza sehemu muhimu kama vyumba na vyoo.
Hii
ni aibu, Tanga ni mjini mkubwa wenye watu wengi wanaopenda michezo, walilie
hilo na kuhakikisha linarekebishika.
Michezo
bila uhakika wa afya ni tatizo, kurekebisha vyumba vya kubadilishia nguo na
vyoo, haiwezi kuwa mamilioni. Uongozi wa Mkwakwani usione raha kupokea tu fedha
za makato ya mapato ya milangoni, badala yake uangalie na huduma inayotolewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment