October 12, 2013


BUKOBA: Kagera walionekana kuwa kiwembe katika dakika za mwisho, lakini mwisho wameshindwa kutegua mtego wa Yanga ambayo inaondoka mjini hapa na pointi zote tatu baada ya kushinda kwa mabao 2-1.


DAR: Pamoja na juhudi za Prisons kushambulia mfululizo, hatimaye dakika 90 zimekamilika bila ya kusawazisha.
Hivyo Simba ikiwa katika uwanja wa nyumbani imefanikiwa kujikusanyia pointi tatu kwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0.
BUKOBA: Ngoma bado nzito, Yanga wanaongoza kwa bao moja lakini Kagera bado wanashambulia mfululizo wakionekana wamepania kusawazisha.
BUKOBA: Dakika ya 62, Hamis Kiiza anaifungia Yanga bao la pili lakini Kagera wanaonekana kuwa wabishi, wanasukuma mashambulizi mengi zaidi huku wakishangiliwa sana kwenye Uwanja wa Kaitaba.


DAR: Ngoma bado ni ngumu, Prisons wanaonyesha uhai zaidi ingawa Simba wanafanya mashambulizi ya kushtukiza.
BUKOBA: Dakika ya 47, Godfrey Wambura anaisawazisia Kagera Sugar. Safu ya ulinzi ya Yanga ilijichanganya.

DAR: Kipindi cha pili kimeanza, Dar es Salaam, Jonas Mkude ameifungia Simba bao la kwanza na timu zinaendelea kushambuliana kwa zamu ingawa muda mwingi zinacheza katikati ya uwanja.

KIPINDI CHA KWANZA:
Katika mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom zinazoendelea, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Simba na Prisons zimemaliza dakika 45 bila ya kupata bao.


Zimecheza kwa kushambuliana kwa zamu na mechi inaonekana kuwa ngumu na timu yoyote inaweza kuibuka na ushindi.

Mjini Bukoba, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Yanga inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Ngassa katika dakika ya 3 tu ya mchezo.


Themi Felix nusura afunge bao katika dakika ya 40 baada ya kupiga tik tak lakini mpira ukatoka nje ya lango kidogo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic