October 13, 2013





Didier Drogba, Salomon Kalou na Gervinho, kila mmoja amefunga bao moja na kuisaidia Ivory Coast kuilaza Senegal kwa mabao 3-1.


Katika mechi hiyo ya kuwania kucheza Kombe la Dunia iliyopigwa jijini Abidjan, bao pekee la Senegal lilifungwa na mshambuliaji we Newcastle, Papiss Cisse.



Burkina Fasso nao wakiwa nyumbani wakaichapa Algeria kwa mabao 3-2 katika mechi ngumu na ya kusisimua.
 
Jibu la timu ipi imesonga mbele litapatikana baada ya mechi za pili, Ivory Coast wakiwa ugenini kama ilivyo kwa Burkina Fasso.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic