October 12, 2013


Hali ya hewa ni baridi na manyunyu kwa mbali, Yanga kiasi Fulani wanateseka kutokana na kuzoea joto la Dar es Salaam.
Lakini kocha wa Yanga, Ernie Brandts amesema hakitawaathiri sana.


“Hali ya hewa ina baridi lakini wakati mwingine jua linatoka, hii haiwezi kuwa shida sana.

“Tatizo moja tu, uwanja ni mbaya sana. Kweli hili suala inabidi lifanyiwe kazi,” alisema.

Kwa upande wa nahodha wa Yanga, Nadir haroub ‘Cannavaro’ naye amelia kuhusiana na uwanja.

“Ukiuangalia kwa mbali unaona una majani safi kabisa, lakini ukiingia utashangaa, hali si nzuri na mambo ni mabaya sana.

“Unacheza ukiwa na hofu ya kuumia, Kagera wenyewe wamezoea lakini kwetu ni hatari. Ila tutapambana na tunataka pointi tatu,” alisema.


Wiki iliyopita uongozi wa Kagera Sugar ulisema hata wao ni wageni kwenye uwanja huo kwani huenda pale kucheza tu na kuondoka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic