Inawezekana kabisa kipindi cha wiki
moja kuanzia leo, ndiyo huwa kigumu zaidi kwa vikosi vya Yanga na Simba.
Timu hizo mbili zimekuwa na hofu
kubwa mara tu zinapomaliza mechi ya mwisho kabla ya ile dhidi ya wao.
Baada ya Simba kumaliza dhidi ya
Prisons na kushinda 1-0, Yanga nao dhidi ya Kagera Sugar na kuilaza 2-1, sasa
macho kwa watani.
Kila upande unatawaliwa na hofu na
lawama zinaanza kwa kila mtu anayepita mbele yao.
Hofu huwa kubwa kwa zaidi ya
asilimia 120, kila upande ukitupa jicho upande wa pili lakini ukifanya ulinzi
mkubwa upande wake.
Hakuna mechi kati ya timu hizo
imewahi kukaribia bila ya pande hizo mbili kutuhumiana katika hujuma.
Yanga wanaamini Simba watafanya
hivyo, Simba vivyo hivyo.
Lakini hata ndani ya klabu hizo, wao
wenyewe hawaaminiani kwa kuwa kila mmoja anaona kama mwenzake anamuuza.
Hii inatokana na makundi ambayo yamo
kila upande wa klabu moja.
Kundi lililo madarakani linakuwa na
hofu, kwamba litahujumiwa hivyo, Simba hawawaamini Simba na Yanga hawawaamini
Yanga.
Kazi katika mechi hiyo inakuwa kubwa
zaidi kwa kuwa kila upande unautuhumu mwingine lakini unajituhumu wenyewe.
Halafu siku ya mwisho, mechi hiyo
inamalizika kwa dakika 90 za kawaida kama ambavyo inaweza kuwa mechi ya Kagera
Sugar au Prisons.
Undugu au urafiki wa watu wengi wa
Yanga na Simba, kipindi hiki huzorota na wengi hukwepana.
Wako wanaohofia kuzungumza na
wengine kwa kuwa wataonekana wamesaliti hasa kama timu itatokea ikafungwa.
Lakini kuna kichekesho zaidi, kama
ikitokea timu moja ikafungwa, hakuna anayeona ni matokeo ya uwanjani, lazima
mzigo uangushiwe kwa mtu au watu fulani.
SIMBA, YANGA, BADILIKENI KWA KUWA
MNAISHI KATIKA KARNE YA 17. TIMU ZENU ZINAWEZA KUSHINDA AU KUSHINDWA BILA YA
KUWA NA HUJUMA.
0 COMMENTS:
Post a Comment