October 13, 2013





Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ametangaza sehemu ya utajili wake kwa kusema ana bonge we mjengo wa ghorofa kama ukibatika kuuona, hauwezi kuamini kama ni wake.


Julio aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kujaribu kuelezea namna watu wanavyomchukulia poa.
“Unajua watu wananichukulia wa kawaida, labda kwa kuwa mimi ni mtu wa watu.

“Ninaweza kuzungumza na mtu yoyote, lakini mimi nina nyumba ya ghorofa ambayo hata ukiiona hauwezi kuamini kama ni yangu.
“Wakati mwingine naangalia tu, maana dharau inazidi na watu hawaelewi. Wakati nacheza wengi wenu (waandishi) hata hamkuniona,” alisema Julio.

Julio anajulikana kwa tambo, mwenyewe amekuwa akisisitiza hivi: “Mimi napenda sana sifa, kama ukiweka sifa na hela, basi mimi nachagua sifa.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic