October 13, 2013

KARIA (MWENYE KOFIA) AKIELEA JAMBO KUHUSIANA NA GARI LAKE KUSHAMBULIWA ALIPOKUWA KITUO CHA POLISI WILAYANI MVOMERO.



Gari la Mwenyekiti wa Ligi kuu, Wallace Karia limeshabuliwa kwa mawe na kuharibiwa vibaya.

Gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser limeharibika hasa vioo ambavyo vimevunjwa na taarifa zinaeleza vurugu hizo zimetokea katika vurugu za wakulima na wafugaji.

Katika vurugu hizo, gari la Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ndilo lilikuwa limelengwa kushambuliwa lakini bahati mbaya mawe yapiga gari la Karia ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomelo.

Karia ndiye aliyeongoza mabadiliko ya kutoka TFF na ligi kuwa chini ya bodi hiyo ambayo hivi karibuni itapata viongozi wapya baada ya uchaguzi.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic