Mchezaji
ghali zaidi wa Real Madrid, Gareth Bale ndiye aliyecheza ovyo kuliko wote
katika mechi ya El Clasico.
Katika mechi
hiyo, Bale aliyenunuliwa kwa pauni milioni 86 ambacho ni kitita kikubwa zaidi
duniani katika uhamisho, alishondwa kung’ara hadi akatolewa kipindi cha pili.
Katika kura
zilizopigwa na mashabiki wa Real Madrid nchini Hispania, wameonyesha Bale ndiye
aliyeshindwa kung’ara.
Katika mechi hiyo ugenini Camp Nou, Madrid ililala kwa mabao 2-1 huku nyota Neymar wa Barcelona aking'ara.
Bale ameshika
namba moja kwa kuboronga kutokana na kura nyingi zilizopigwa dhidi yake.
Lakini bado
mashabiki hao wakasisitiza wanaamini ana muda wa kufanya makubwa.
Mashabiki wa
Madrid wamekuwa tofauti na uongozi wao, kwani wana uvumilivu mkubwa na
wamekubali kutoa muda kwa Bale ambaye ameshindwa kuonyesha cheche zake mapema.
0 COMMENTS:
Post a Comment