Wanachama wa Yanga wamepewa muda wa
mwezi mzima kupiga kura ya kuamua klabu yao kuendeshwa kwa mfumo wa kampuni au
la.
Utaratibu huo unaanza leo hadi Novemba
10, mwaka huu na Katibu Mkuu, Lawrence Mwalusako ameeleza boksi maalum la
kupigia kura limewekwa makao makuu ya klau hiyo.
“Kila mwanachama afike akiwa na kadi
yake ya uanachama kwa ajili ya kazi hiyo ya kupiga kura. Hii itasaidia watu
kutopiga kura mara mbili,” alisema.
Katika mkutano wa Januari, mwaka huu
wanachama walipewa pendekezo la kuchagua kuhusiana na kampuni au mfumo wa sasa
na mwenyekiti wa kamati ya utendaji akawaeleza kwamba atawapa nafasi ambayo
sasa imetolewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment