RAGE |
Wiki iliyopita nilipokea makala ya Mwenyekiti wa Simba,
Ismail Rage kupitia email, aliomba yachapishwe kwenye Gazeti la
Championi ili ajibu Hoja Yangu niliyokuwa nimeandika siku kadhaa nyuma. Nikakubali
ombi lake, PIA NINAYATOA KWENYE
SALEHJEMBE KWA KUWA NILIANZA KUTOA HAPA KUANZIA MAKALA NILIYOMCHAMBUA, ALIYOJIBU NA HII.
SALEHJEMBE KWA KUWA NILIANZA KUTOA HAPA KUANZIA MAKALA NILIYOMCHAMBUA, ALIYOJIBU NA HII.
Baada ya kusoma vizuri, nikatabasamu na kugundua mambo
mawili mapema kabisa. Kwanza, uandishi wa makala hayo, nikagundua ni mmoja wa
waandishi chipukizi ndiye alipewa kazi ya kuiandika baada ya kusikiliza maneno
ya Rage bila ya kuyapima, nikashangazwa, lakini ni suala la ajira, siwezi
kumlaumu ingawa iko siku nitamfikia.
Pili, hoja laini za Rage ambaye hata alichokisema,
kilinithibitishia kwamba kila ninachoandika kuhusu yeye, kamwe sijawahi
kukosea. Waswahili wanasema hivi, “ukimya ni jibu la mjinga”.
Lakini inapofikia wakati unalazimika kusema kwa
maslahi ya michezo ya taifa letu, basi hakuna haja ya kunyamaza. Safari hii
umemuona Rage ameamua ‘kuandika’ makala na hii ni baada ya kuona sibabaiki na
lawama na vitisho vyake, kupitia watu mbalimbali ambavyo amekuwa akivitoa
kujaribu kuninyamazisha, kitu ambacho naona anapoteza muda wake.
Naweza kumpongeza kwa kuona umuhimu wa kuzungumza,
wenye uwezo wa kuchambua mambo huyachambua na wasioweza hutumia vitisho kwa
kuwa hawawezi kujibu hoja za msingi, hata hivyo Rage amejaribu kujibu hoja ya
msingi bila tafakuri, akionyesha wazi ni mtu mroho wa madaraka, asiye na huruma
hata kidogo na maendeleo ya Simba na badala yake maendeleo binafsi. Kuna vingi
vya kuthibitisha hilo.
Wakati akifafanua katika makala yake, eti Rage
alijisifia kufanya biashara ya kumuuza Emmanuel Okwi katika Klabu ya Etoile Du
Sahel kwa dola 300,000 (Sh milioni 480) ambazo ameifanya kwamba yeye ni mtu
makini na ana uzoefu na biashara ya wachezaji! Nilijiuliza huyu Rage ni mzima
kweli? Naamini atakuwa ana tatizo.
Mimi niliita biashara kichaa kwa kuwa hakuna fedha
iliyoingia Simba hadi sasa huku Okwi akianza kurushwa kama mpira, sasa atacheza
SC Villa kwa miezi sita. Kwa kipindi hiki Simba inafaidika nini, kama si
biashara kichaa ni nini? Yeye anashangaa akitoa mfano wa kitu kilichonunuliwa
kwa Sh 1,000 kikiuzwa Sh 1,500 kama inaweza kuwa biashara kichaa. Kweli haiwezi
kuwa, sasa Simba wamemuuza Okwi au wamemgawa?
Kuonyesha Rage ni mbabaishaji kama ambavyo nimekuwa
nikisema siku zote, alijisahau na kudanganya kwamba eti Okwi kama asingeuzwa
kipindi hicho, angeondoka na kujiunga na timu nyingine kama Yanga au Azam FC
kwa kuwa mkataba wake umebakiza siku chache.
“Ukiwa muongo, usiwe mwepesi kusahau”. Naona amesahau
kwamba alipewa fedha dola 40,000 (Sh milioni 64) na kwenda Kampala, Uganda
kumsainisha Okwi mkataba wa miaka miwili, kama kawaida yake yeye akachukua
ujiko kama muhusika mkuu.
Bado nasisitiza kuwa ile ni biashara kichaa na
ninaweza kufafanua hivi, kwamba hakuna ambacho Simba inafaidika katika mauzo ya
Okwi zaidi ya ‘stress’ za kuendelea kudai, huku ikipata hasara ya kupiga simu
au kusafirisha watu kwenda kudai fedha zao Tunisia.
Hakuna mfanyabishara mwenye malengo anaweza kufanya
ujinga wanaofanya Simba katika kipindi hiki kwa kuwa wanaendelea kupoteza muda
na hii yote inatokana na Rage, kama angekuwa makini siku husika ya biashara,
basi leo Simba isingekuwa ikihagaika na kupoteza fedha kama ilivyo sasa.
Wakati Simba inamuuza Okwi ilikuwa inashiriki michuano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mganda huyo alikuwa tegemeo katika kuanzisha
mashambulizi. Ikamuuza, halafu haikupata hata shilingi, hilo likachangia timu
kuzorota na mwisho kuambulia vipigo vya aibu kutoka kwa FC Liboro ya Angola
ikiwa nyumbani ikalala 1-0 na ugenini 4-0. Bado Rage anaona hiyo ni biashara
safi sana.
Kama faida, basi Simba ingepata fedha kipindi kile kwa
kuwa ilikuwa inazihitaji sana kujiimarisha, ikashindikana. Hadi leo
haijazipata, lakini Rage anaiita biashara na tena anajisifia, kweli duniani,
kila mmoja ana uwezo wake tofauti wa kufikiri!
Kilichomuuma ni mimi kusisitiza kwamba fedha za Okwi
ziondoke na kichwa cha mtu, ndiyo maana kwa kiongozi makini anaweza kujipima
kwa kosa kubwa moja na kuona kweli anastahili kujiuzulu kwa maslahi ya
anachokiongoza, najua Rage hawezi na ndiyo maana anasifia madudu aliyoyafanya akilazimisha
kioo kiwe almasi, kitu kisichowezekana hata iwe vipi.
Anasema Simba wamekuwa na mafanikio sana, wamechukua
makombe tena alivyo msahaulifu anakumbushia hadi Kombe la BancABC ambalo timu
ya vijana ya Simba ambao aliwazungusha kuwapa fedha zao za ubingwa
walizoahidiwa na hadi leo bado kuna fedha ambazo hawajalipwa. Huyu jamaa mzima
kweli?
Lakini ajabu, katika makala hayo, Rage alijisifia eti
si wao Simba tu ambao wanaidai Etoile du Sahel akitolea mfano wa timu nyingine,
akiwemo wakala Msenegali. Sasa Simba linawahusu nini!
Hao Wasenegal wanapaswa
kuangalia yao na Simba yake, unajisifia kuingia kwenye matatizo eti kwa kuwa na
wengine pia wamo humo, ehh! Huyo ndiyo Rage bana!
Rage amekuwa ni mtu wa kufeli karibu kila anachohusika
kama lile suala la kumsainisha Mbuyu Twite jijini Kigali, Rwanda, mwisho
akaishia kutumia picha aliyopiga naye akiisambaza kwenye mkutano wa wanachama
wa Simba, kuonyesha alivyofanikiwa.
Haikutosha hapo, akaibandika kwenye mtandao
wa kijamii wa Facebook, halafu siku chache baadaye beki huyo akatua Yanga, huku
akisema alipiga picha na Rage kama shabiki wa kawaida! Kumbuka Simba ilipata
hasara, tiketi ya ndege na baadhi ya fedha, lakini aibu kwa kuonekana
mwenyekiti wake anafanya mambo ya kubahatisha, kwake si tatizo, maana amezoea
kubahatisha.
Leo kamuuza Okwi, hadi hapa unaposoma makala haya,
Simba haijapata hata senti tano ya malipo ya fedha hizo, yeye anajisifia na
kuona amefanya biashara kwa uzoefu mkubwa! Tena kwa tambo huku akisema eti
ninapaswa kufanya utafiki kwanza, la sivyo nitakuwa kasuku!
Ametoa mfano wa kauli hiyo ya Mwenyekiti Mao, bila ya
kujua aliitumia katika sehemu isiyo sahihi, karukia maneno kutokana na
umasikini wake wa maneno ya Kiswahili (sababu anaijua).
Ukweli suala hilo wala halihitaji uchunguzi, ukweli ni
kwamba Simba imefanya biashara ya dola 300,000 hadi sasa haijapata kitu na
hakukuwa na haja ya haraka kwa kuwa Okwi tayari aliongeza mkataba na Simba na
kama Waarabu hao walisema hawana fedha, basi Okwi angebaki na kuendelea
kuitumikia timu yake hadi miezi michache baadaye katika dirisha
litakapofunguliwa tena wangekuja kumnunua wakati wana fedha. Sasa nini cha
kuchunguza hapa?
Siku moja niliwahi kumpigia simu Rage na kumuuliza
hivi, kwamba nina taarifa kuwa akiwa Tunisia alifanya mambo mawili ya kijinga.
Kwanza, Etoile walitangaza kumnunua Okwi kwa dola 500,000 (Sh milioni 800), akiwa
huko yeye akawataarifu baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji kwamba bei
imepungua hadi kufikia dola 300,000.
Lakini taarifa zikaeleza katika dola 200,000
iliyopunguzwa, Rage ‘alikatiwa’ asilimia 10, yaani dola 20,000 (Sh 32m) kama
shukurani ya kukubali kupunguza hiyo bei. Pili, kukawa na taarifa kwamba
alikuwa akimuomba fedha Okwi mara tu baada ya mchezaji huyo kulipwa mamilioni
kama fedha zake za kukubali kuingia mkataba na Etoile. Rage akaniambia maneno
yote hayo ni uzushi, sikuridhika kwa dhati, ila nikaachana nayo.
Lakini bado nikabaki na hofu kwa kuwa mwenendo wake na
hasa maneno yake ya kubabaisha, yakazidi kunibabaisha. Huyu mtu ni tatizo
katika mchezo wa soka nchini na si Simba tu.
Ingekuwa ni kutumia neno kasuku, basi yeye ndiye
angeendana na kila kitu, kwamba ana maneno mengi mazuri lakini katika
utekelezaji ni tatizo kubwa na ana uwezo mkubwa wa kusema maneno kwa mbwembwe,
utekelezaji wake ni sifuri.
Angalia mambo ya ujenzi wa uwanja, kuna mengi tu
ambayo yanaweza kuwa sehemu ya kuonyesha madudu wakati wa uongozi wa Rage.
Makocha wawili Wazungu katika msimu mmoja, mmoja
akalazimika kupata msaada wa kulipa, mwingine hadi sasa yuko jijini Dar akihaha
kulipwa. Nitaishia hapa, nitampa nafasi Rage aendelee kutoa anazoziita hoja
zake, halafu nitahamia katika upande huo wa makocha, ujenzi wa uwanja, namna
anavyong’ang’ania fedha za tiketi ili apate ‘pasu’ na mengine mengi ambayo
kabla sikuwahi kuyagusa ili kuwaonyesha kiasi gani kuwa mtu huyu mheshimiwa ni
chui mwenye ngozi ya kondoo, mwenye maneno matamu kama chiriku lakini mwenye
hamu kubwa ya kuitumikia nafsi yake tu.
Duh Natamani nami niwe mwandishi au nimiliki Blog, Inawezekana bwana Salehe ukawa mganga wa Kienyeji, Yaani baada ya kusoma tu makala ukagundua ameandikiwa? mimi nilisoma ila sikugundua hilo. Ugomvi wenu usitutukanishe sisi Simba.... Ujinga mnao nyie mnaolumbana na si Simba kama ulivyo andika hapo juu. ... Angalia anayekutuma sisi simba hatuna mpango nae. ENDELEA Kupiga promo alafu majibu tutakupatia muda ukifika.
ReplyDeleteIt is better to take the massage rather than disgracing somebody....
ReplyDeleteapo salehe unaonesha unamahaba na kandambili wewe acha unazi
ReplyDeleteWewe Salehe unapotuandikia ujinga wako kumkashifu huyo Rage inakusaidia nini!!!! unaonyesha jinsi ambavyo hujaelimika wewe kama mwandishi na kiji-blog chako ndo unatumia kutukana watu na kuporomosha matusi!!!. Acha ujinga acha kutafuta miji-sifa isiyo na sababu za msingi, Rage ni sawa na baba yako unapomporomoshea matusi hayo yote inakusaidia nini!!!? Acha ujinga kama unajua sana maneno ya kiswahili si ukaimbe taarabu mtaani!
ReplyDeleteUkubwa si kichwa bali ni akili. Hutofautiani na na mjinga mwenzio mmoja alikuwa akioga bwawani kavua nguo zake kaacha mara mwehu mmoja akapita na kuzichukua mjinga mwenzio kuona nguo zake zimechukuliwa si katoka majini hivyo hivyo akiwa uchi na kuanza kufuka mwizi wa nguo zake, sasa na wewe unako elekea ni huko. yangu ni hayo wajinga wenzio watakutia moyo wenye akili watakuona mjinga tu
Nikweli kabisa salehe huna jipya dogo! unaachakuomba kazi jangwani wewe unakuja uomba kazi msimbazi acha hizo sisi hatukutaki, tuache na ujinga wetu.kwani mpaka sasa samba umeona tumeomba pesa kwa mtu? .We ni mtaalamu wa mashairi nenda jangwani ukawatungie wakacheze kidole juu.
ReplyDeleteMi naona angalia mambo yako si kuingilia masuala ya samba,we sio msemaji wa samba.