Mshambuliaji nyota wa Simba, Amissi
Tambwe amesema yeye ni muumini wa dini ya Kikristo tokea kuzaliwa kwake ndiyo maana alionyesha ishara ya msalaba baada ya kufunga bao.
Tambwe raia wa Burundi ameiambia blogu
hii kwamba jina la Amissi limekuwa likiwachanganya wengi, lakini ni la ukoo na
alipewa akiwa mdogo.
“Hili ni jina langu tokea nikiwa mtoto,
watu wamekuwa wakilichanganya sana na wanadhani ni Muislamu, lakini hapana,”
alisema.
Mkanganyiko wa kuwa Tambwe ni muumini wa
dini gani baada ya kufunga bao lake la nane katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana.
Baada ya kufunga bao hilo, Tambwe
alionyesha ishara ya msalaba, hali iliyoonyesha kuwachanganya wengi waliokuwa
wakiamini ni Muislamu.
Tambwe amefunga mabao nane katika mechi
sita za Ligi Kuu ya Vodacom na ndiye anaongoza kwa wapachika mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment