Uongozi wa
Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, imesema bado inaamini Shadrack
Nsajigwa ni kocha wao.
Nsajigwa,
hivi karibuni aliripotiwa kutangaza kuitosa timu hiyo kutokana na kushindwa
kuwajali wachezaji wake.
Katibu Mkuu
wa Lipuli, Wile Chikweo, amesema wanashangazwa na taarifa zilizoenea kuwa
Nsajigwa ameikimbia timu hiyo.
Amesema wao
wanajua yupo nyumbani kutokana na matatizo ya kifamilia na hajawajulisha kuhusu
kuachana na kazi.
“Tumekuwa tukisikia kwenye vyombo vya habari
kuwa Nsajigwa kaondoka, sisi bado tunamtambua kama kocha wetu, maana ana
mkataba wa maandishi, hatujavunja mkataba wake.
“Aliomba
ruhusa kwenda kumuuguza mama mzazi, akisema hakuwa na muuguzi, mpaka leo (jana)
hajatutaarifu chochote kuwa ameachia ngazi,” alisema katibu huyo.
Kabla ya
Nsajigwa kutangaza kuachia ngazi, Lipuli ilikuwa imepoteza michezo mitatu
mfululizo ya Ligi Daraja la Kwanza na nyota huyo wa zamani wa Yanga akasema
timu haiwezi kufanya vizuri kwa kuwa haiwajali wachezaji wake, hivyo ameamua
kujiweka kando.
Kwa sasa timu
hiyo ipo chini ya kocha Fide Kalinga ambaye anakaimu na wiki iliyopita
aliiongoza kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji.
Nsajigwa
alipotafutwa na Championi Jumatatu jana simu yake ilikuwa ikiita kwa muda mrefu
bila kupokelewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment