Rais wa TFF anayemaliza muda wake,
Leodeger Chilla Tenga amesema amecha milango wazi kwa ajili ya mteule, Jamal
Malinzi.
Tenga amesema kwa kuwa amekaa miaka nane
TFF hivyo hawezi kutokea mtu akasema hawezi kumsaidia Malinzi.
“Nampongeza Malinzi na wote walioshinda.
Niko tayari kumsaidia, nitaacha milango wazi kwa ajili yake na wakati wowote
anaweza kuja na tukajadili jambo,” alisema.
“Wajumbe waliopiga kura pia wanastahili
pongezi kubwa kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kwa ajili ya uchaguzi huo
muhimu,” alisema Tenga.
Mara baada ya Malinzi kushinda, Tenga
alimkabidhi mpira na katiba, huku akisisitiza makabidhiano ya ofisi yatafanyika
Jumamosi saa 5 asubuhi katika makao makuu ya TFF, Karume, Ilala jijini Dar es
Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment