Rais anayemaliza muda wake katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodeger Tenga atakuwa madarakani kwa siku saba nyingine.
Tenga amesema atakabidhi ofisi kwa Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi Jumamosi ijayo.
Tenga ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwa Malinzi na uongozi wake mpya kwa lengo la kuendeleza uongozi wake ulipiishia.
Tenga aliwapongeza wajumbe pamoja na walioshinda na kutaka mshikamano uendelezwe kwa ajili ya kulisaidia shirikisho hilo kuendeleza mpira nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment