Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai
limemuomba radhi mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Amissi Tambwe raia wa
Burundi straika huyo ameibuka na kudai ni waongo.
Tambwe alifunga mabao manne katika mchezo dhidi
ya Mgambo Shooting, Septemba 18 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa na kunyimwa
mpira kama zawadi baada ya mechi kumalizika.
Ofisa Habari
wa TFF, Boniface Wambura amesema wamemuomba radhi straika huyo kutokana na
kutopewa mpira huo licha ya kuwa suala hilo halipo kwenye sheria za Shirikisho
la Soka la Kimataifa (Fifa).
Alisema waliamua kumuomba radhi kama ‘fair play’
lakini walimtaarifu aufuate katika ofisi
za shirikisho hilo na pia mwamuzi aliyemnyima mpira huo hawezi kuadhibiwa.
“Tulimuomba radhi kutokana na tukio lile na
tulimtaka aje kuchukua mpira wake nafikiri atakuwa anajipanga ili aje kuchukua
siku yoyote,” alisema Wambura.
Championi lilienda mbele na kumtafuta straika huyo
anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi kuu kwa sasa akiwa ameshatupia nane
wavuni ambapo alidai hajafuatwa na mtu
yeyote kuhusiana na suala la kupewa mpira na hafikirii tena suala hilo.
“Sijafuatwa na mtu yeyote na wala sina wazo
lolote kuhusiana na ishu hiyo ya mpira na kama wataamua wenyewe kuniletea au
wakiukabidhi kwa viongozi wangu sawa tu nitauchukua,” alisema Tambwe na
kuongeza:
“Naumwa maralia tokea jana na sijfanya
mazoezi yoyote kwa kuwa mwili unaniuma
sana.”
0 COMMENTS:
Post a Comment