October 8, 2013




Leo Messi ameonekana yuko fiti kabisa na anatarajia kurejea katika kikosi cha Barcelona.


Messi alikataa kusafiri na timu yake ya taifa ya Argentina ili apate matibabu na baadaye kuanza mazoezi ya taratibu kitu ambacho amefanikiwa.

Yeye mwenyewe ametuma picha katika moja ya mitandao ya kijamii akionyesha picha wakati akipimwa na daktari wa timu hiyo kuangalia kama anaweza kuanza mazoezi na wenzake.

“Sasa mambo safi na ninaanza mazoezi,” aliandika baadaye.
Inaelezwa kwamba ataanza mazoezi na wenzake leo usiku au kesho asubuhi na rasmi anatarajia kurejea na kukichezea kikosi cha Barcelona chini ya Tata Martino siku ya Oktoba 19 wakati wakiivaa Osasuna.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic