October 9, 2013





Kocha  Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts, amesema bado hajasaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo kwa kuwa bado haujafika mezani kwake.


Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi aliyetua Yanga kwenye msimu wa 2012/13 akitokea APR ya Rwanda, amesema anashindwa kumwaga wino klabuni hapo kwa kuwa bado hajauona mkataba husika na kuweza kuchambua baadhi ya vipengele.
 
 Brandts ambaye ni beki wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, alisema anachohitaji kwa sasa ni kuwekwa mezani kwa huo mkataba halafu aangalie kila kipengele kisha ataamua kuusaini au la.

Aliongeza kwa kusema kuwa, yeye hana tatizo na muda wowote yupo tayari kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga lakini hayo yatakuja baada ya mkataba kuwekwa mikononi mwake na kuupitia.

“Sijasaini mpaka sasa, kikubwa ni kwamba sijauona mkataba niupitie, sina tatizo kama nitapewa niupitie na mimi nitoe maoni yangu juu yake, lakini siwezi kukijadili kitu ambacho sijakiona,” alisema Brandts. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic