England imefanikiwa kuibuka na ushindi
wa mabao 4-1 dhidi ya Montenegro katika mchi yao ya kuwania kucheza Kombe la
Dunia nchini Brazil, mwakani.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye
Uwanja wa Wembley na kumalizika hivi punde, mabao ya England yalifungwa na
Wayne Rooney, beki wa Montenegro akajifunga, kinda Townsend akapiga la tatu
kabla ya Sturridge kujiangusha na kupata penalty aliyoikwamisha wavuni.
LUKAKU AKIFUNGA BAO LA KWANZA, MABAO YAKE YAMEIPELEKA UBELGIJI KWENYE KOMBE LA DUNIA |
Wakati England inashinda mabao hayo,
Sweden ikiwa nyumbani ililazimika kusubiri hadi dakika ya 86 kupata bao la pili
na la ushindi lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic.
Mechi hiyo dhidi ya Austria ambayo
pamoja na kuwa wageni walitangulia kupitia Martin Hank, Martin Olsson
akasawazisha na Zlatan akamaliza kazi.
MODRIC NA HAZARD WAKIWANIA MPIRA |
HAZARD KAZINI... |
Upande mwingine, Uholanzi imeishindilia
Hungry kwa mabao 8-1 huku mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie
akipiga mabao matatu yaani Hat trick. Mabao mengine ya wenyeji yalifungwa na
Strootman, Jeremain Lens, van der vaart na Arjen Robben.
Ujerumani nayo ikaichapa Ireland kwa
mabao matatu huku Sami Khedira, Andre Schurrle wa Chelsea na Mesut Ozil wa
Arsenal wakipachika mabao hayo matatu.
Urusi wakiwa ugenini wakaiangusha
Luxembourg kwa mabao 4-0. Slovenia ikaiagunia Norway kwa 3-0, Iceland
ikaitandika Cyprus 2-0 na Uturuki ikicheza ugenini ikashinda 2-0 dhidi ya
wenyeji Estonia.
Italia ikiwa ugenini imelazimisha sare
ya 2-2 dhidi ya Denmark, Coratia ya kina Modric imelala nyumbani 2-1 dhidi ya
Ubelgiji na Romelu Lukaku ndiye muuaji aliyepiga zote na kuipa timu yake ya taifa nafasi ya kwenda World Cup. Mara ya mwisho, Ubelgiji ilicheza michiano hiyo mwaka 2002 ilipofanyika Japan na Korea Kusini.
Wales ya kina Bale
ikailamba Macedonia 1-0 na Jamhuri ya Czech ikaipindua Malta kwa kuichakaza kwa
bao 4-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment