Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
imewarejesha warufani wote watatu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Kamati
mpya ya Utendaji ya TFF utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Samwel
Nyalla, Ayubu Nyaulingo na Ayoub Nyenzi walikata rufani mbele ya Kamati hiyo
inayoongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bernard Luanda kupinga
uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaondoa katika uchaguzi huo ambapo wote
wanagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda mbalimbali.
Akisoma
uamuzi wao leo (Oktoba 11 mwaka huu) mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ofisi
za TFF, Jaji Luanda amesema baada ya kusikiliza hoja za Mrufani Nyalla
walipitia Kanuni za Uchaguzi za TFF na kugundua yafuatayo;
Ibara
ya 10(3) imeweka masharti makuu mawili ya ujazaji wa fomu za kugombea uongozi.
Fomu hiyo ni lazima iwe na saini ya mgombea na ni lazima ithibitishwe na
viongozi wa shirikisho.
Kamati
imepitia Kanuni za Uchaguzi haijaona sehemu fomu hiyo ya uongozi
imeambatanishwa ili kuifanya kuwa Kanuni ya Uchaguzi. Ni maoni ya Kamati kuwa
ni vizuri fomu za kugombea zikawa ni sehemu ya Kanuni za Uchaguzi.
Kwa
vile Kanuni za Uchaguzi za TFF za 2013 pia hazijaainisha nini adhabu kwa
mgombea aliyekosea kujaza Fomu namba 1 ya kugombea uongozi, Kamati inaona
itakuwa si haki kumnyima mgombea nafasi ya kushiriki katika uchaguzi kwa vile
tu fomu yake haijajazwa vipengele vyote.
Nyalla
aliondolewa kwenye uchaguzi na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa maelezo kuwa si
mtu makini anayeweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu baada ya kushindwa
kujaza Fomu namba 1 kipengele cha 15 kinachohusu malengo ya mgombea uongozi.
Kwa
upande wa Nyaulingo ambaye aliondolewa kwa kukosa uzoefu uliothibitika
kulingana na Ibara ya 29(3) ya Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF, Kamati ya Rufani imeamua ifuatavyo;
Kamati
ya Rufani ya Uchaguzi imepokea sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza
hoja na maelezo kutoka kwa Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi
wa Kamati ya Uchaguzi.
Mrufani
alifafanua historia yake katika masuala ya michezo kuanzia alipokuwa anasema
Chuo Kikuu kuanzia 2005-2009 na pia ushiriki wake kama mchezaji wa Rukwa United
iliyowahi kushiriki Ligi ya Mkoa wa Rukwa na ligi nyingine za kitaifa.
Kwa
kusoma maana ya ‘Familia ya TFF’ iliyoko kwenye utangulizi wa Katiba ya TFF,
pamoja na Ibara ya 29(3) na 29(6) ya Katiba hiyo, Kamati imejiridhisha kuwa
Mrufani ana sifa za kugombea uongozi wa Shirikisho na amekidhi kigezo cha sifa
za ugombea.
Ameshiriki
kwenye mchezo wa mpira wa miguu kama mchezaji na mtawala, hivyo kutimiza kigezo
kilichohitajika cha ushiriki katika uongozi na utawala wa mchezo wa mpira wa
miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.
Kwa
kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani.
Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani anapewa nafasi ya
kushiriki katika uchaguzi.
Kuhusu
Ayubu Nyenzi aliyeondolewa kwa kukosa uzoefu kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya
Katiba ya TFF na Kanuni ya 9(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, na pia kushindwa
kuthibitisha uraia wake mbele ya Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani katika
uamuzi wake imesema;
Imepokea
sababu za rufani na imepata fursa ya kusikiliza hoja na maelezo kutoka kwa
Mrufani juu ya sababu zake alizozitoa kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi.
Baada
ya uchambuzi wa kina, Kamati imeona kuwa kulingana na maelezo yaliyotolewa na
Mrufani na viambatanisho vilivyowasilishwa, Kamati haina shaka kuhusu uraia
wake. Uthibitisho wa uraia unapaswa kufanywa kwa umakini na taasisi yenye
mamlaka ya kiserikali kufanya hivyo.
Kamati
pia imejiridhisha kupitia Fomu namba 1 iliyojazwa na kusainiwa na Mrufani kuwa
kuanzia mwaka 2004 mpaka 2010, Nyenzi ameshika nyadhifa za utawala wa mpira wa
miguu na hasa katika klabu ya Yanga, uzoefu unaomfanya kuwa na sifa ya kugombea
nafasi ya uongozi katika TFF kulingana na Ibara ya 29(3) ikisomwa pamoja na
Ibara ya 29(6).
Kwa
kuzingatia hayo, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi inaruhusu rufani ya Mrufani.
Uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi umetenguliwa na Mrufani atashiriki katika uchaguzi
wa TFF kwa nafasi anayogombea.
Wakati
huo huo, Kamati ya Rufani ya Maadili ya TFF
inakutana keshokutwa (Oktoba 13 mwaka huu), kufanyia mapitio (revision) ya
uamuzi wa Kamati ya Maadili kwa waombaji uongozi wanane kama ilivyoombwa na
Sekretarieti ili kutoa mwongozo wa utekelezaji wa uamuzi huo
0 COMMENTS:
Post a Comment