JUMANNE CHALE |
Kocha wa Prisons wa Mbeya,
Jumanne Chale amesema kipigo walichokipata cha mabao 2-1 dhidi ya Ashanti
United leo ni uzembe.
Chale amesema kikosi chake ni
bora na kilikuwa na uwezo wa kushinda mechi hiyo kama wangejituma.
“Tulitakiwa kujituma na kujua
kwamba tuna uwezo na kikosi kizuri, tumezembea na hili ni fundisho,” alisema.
Lakini awali, kocha huyo
alionyesha kutofurahishwa na hali ya mwamuzi kwamba alionekana kuwaminya kiana.
Ashanti United imeibuka na
kushinda mechi ya pili huku ikiwashtua wengi, kwani ilikuwa haijashinda mechi
yeyote tokea kuanza kwa ligi hadi ilipoichapa Coastal Union kwa idadi hiyo ya
mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment