November 17, 2013



 
AFANDE SELE AKIWA NA MBUNGE WA KAWE (CHADEMA), HALIMA MDEE
Rasmi leo msanii maarufu wa hip hop, Afande Sele amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Afande ameonyesha ni mwenye furaha na kwenye mtandao wa Facebook ameweka maneno haya.

Hakuna kusanda,hakuna kumbwanda,mbele kwa mbele makamanda,vua gamba vaa gwanda kisha kaza mkanda, wanashuka sisi tunapandaaa,,,,Leo tunaanza kuandika hisyoria mpya ktk mkoa wetu wa morogoro na tz kwa ujumla kwa sababu nikiwa kama msanii wa muda mrefu na mfalme pekee wa mzk wa kizazi kipya ninaetunga nyimbo zangu kwa kuzingatia ujumbe muhimu ktk jamii kwa mambo ya kisiasa,kiuchumi,elimu,amani na upendo nk,sasa leo nimeamua kwa ridhaa yangu iliyosukumwa na uzalendo na mapenz makubwa kwa taifa langu kuchukua kadi ya kujiunga rasmi uanachama wa CHADEMA,tukio hilo kubwa litafanyika leo jioni ktk mkutano wa hadhara utakaofanyika kata yetu ya mafiga/misufini na utahudhuriwa na viongoz mbalimbali wa chama kutoka makao makuu ya chama dsm pamoja na mbunge wa nyamagana mh ezekiel wenje,kwa wakaz wa moro wazalendo nyote mnakaribishwa saaana,ahsanteni wana'ndugu,siasa si uadui,tupingane/tusipigane,Pendo moja!

1 COMMENTS:

  1. Dalili za kushindwa kasi ya vijana kwenye muziki wa bongo na Hip pop ndio imewakimbiza wakongwe wa muziki huo na kwenda kwenye siasa lakini anguko la maisha huenda likaanzia hapo maana shida ni ubunge tu.

    Emma James

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic