November 15, 2013





Wakati burudani ya Ligi Kuu England ikiendelea, pamoja na ushabiki wa timu kubwa au maarufu kama Arsenal, Manchester United, Chelsea na Manchester City kuwa kipaumbele, lakini zinaonekana kufeli katika mambo kadhaa.


Ikiwa ni kila baada ya timu kucheza mechi 11, inaonekana Aston Villa ambayo imekuwa ikiwashangaza wengi msimu huu, ndiyo timu yenye ngome ngumu zaidi.


Katika mechi hizo 11, Southampton imeruhusu mabao matano kutinga katika nyavu zake, hali ambayo imeisaidia kuwa katika tano bora na inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 22.

Angalau Arsenal, Chelsea na Liverpool ambazo pia ziko katika tano bora zimeonyesha kuwa na ngome nguvu, tena zinazofanana kwa mwendo, kwani zote zimeruhusu mabao 10 katika mechi hizo 11.

Manchester United inayoshika mkia katika tano bora, bado inaonekana kutokuwa imara sana kwani katika mechi hizo 11, imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13.

Lakini hilo si suala kubwa sana, ishu zaidi ni katika takwimu za kila mechi, kwamba timu ilicheza bila ya kufungwa hata bao moja ‘clean sheet’, hii ni bila ya kujali imeshinda au kufungwa.

Timu kubwa au maarufu kama Man United, Arsenal na Chelsea zimefeli kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na ngome ambayo inaweza kuizuia timu nyingine kumaliza mechi bila ya kufungwa hata bao moja.

Katika mechi 11 zilizocheza, timu hizo zimetoka katika mechi tatu tu bila ya kufungwa bao hata moja, hivyo kuzifanya zishike nafasi ya chini ya kuwa timu zinazoaminika kwa kuwa na ngome ngumu yenye uhakika wa kuzuia nyavu zake kutoguswa kabisa.

Ubora wa ngome wa timu hizo tatu katika suala la kuzuia kutofungwa hata bao moja kwa kila mechi zinazocheza ni 27.3%, wastani ambao unashika nafasi tatu za chini.

Crystal Palace na Sunderland ambazo ziko mkiani mwa ligi hiyo, ndiyo timu ambazo zina uwezo mdogo kabisa wa kuzuia zisifungwe hata bao moja kwa mechi zinazocheza. Katika mechi 11, zilitoka uwanjani bila ya kufungwa hata bao moja katika mechi moja tu ambao ni wastani wa 9.1% na ndiyo wa chini kabisa.

Fulham inafuatia, inashika nafasi ya pili kwa wastani mbaya wa clean sheet, katika mechi 11, ni mbili tu haikufungwa hata bao moja na ina wastani wa 18.2.

Ingawa inashika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 20 ambazo ni sawa na zile za Man United na Everton, Tottenham ndiyo timu inayomiliki ngome ngumu zaidi kwa kuwa katika mechi 11, imecheza 7 bila ya kuruhusu hata bao moja na wastani wake wa ubora ni 63.5%.

Southampton, Everton na West Ham ndizo zinazoshika nafasi ya pili kwa ubora wa kutoruhusu hata bao moja katika kila mechi, kwani katika 11 zilizocheza, zilitoka uwanjani mara sita nyavu zao zikiwa hazijaguswa. Wastani wao ni 54.5%.

Katika vigogo, Liverpool inaungana na Aston Villa, Newcastle Utd, Manchester City, Swansea City na  Wes Brom kwa kuwa timu yenye wastani wa 36.4% kwa kucheza mechi 11, kati ya hizo zikatoka uwanjani mara nne bila ya kufungwa hata bao moja.

Katika soka pointi ndiyo suala muhimu la kwanza, baada ya hapo unaangaliwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa. Maana yake timu ambazo zinaweza kucheza mechi bila ya kufungwa hata bao moja, zinakuwa na uhakika katika wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa ambao ni muhimu.

Mara nyingi hutokea timu zikalingana pointi, iliyokuwa makini katika kutoruhusu ngome yake kutikiswa kirahisi inakuwa na nafasi ya kuwa juu ya nyingine ambayo haikuwa na ngome imara au hesabu bora za kuruhusu mabao.

Kimahesabu, makocha Arsene Wenger, Jose Mourinho na David Moyes wapo katika changamoto kwa kuwa Liverpool, Tottenham, Southampton na Manchester City zinaweza kuwasumbua baadaye kama itatokea wakalingana mabao ya kufunga.


            CS
Pld
Perc.
7
11
63.6%
6
11
54.5%
 Everton 
6
11
54.5%
6
11
54.5%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
4
11
36.4%
3
11
27.3%
 Arsenal 
3
11
27.3%
3
11
27.3%
3
11
27.3%
 Chelsea 
3
11
27.3%
3
11
27.3%
 Fulham 
2
11
18.2%
1
11
9.1%
1
11
9.1%

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic