November 27, 2013



 
LUHENDE AKIWA MAZOEZINI JANA KABLA YA BRANDTS KUAMUA AFANYE MAZOEZI YA PEKE YAKE
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amemuweka kando beki wake David Luhende ili afanye mazoezi pekee.
 
Luhende amewekwa kando kutokana na kuwa na maumivu na Brandts amemtaka afanye mazoezi pekee. Awali Luhende alianza mazoezi pomoja na wenzake lakini baadaye Brandts akamtoa na kumtaka akimbie peke yake.

Wakati wenzake walikuwa wanafanya mazoezi pamoja, Luhende aliendelea kuzunguka uwanja taratibu.

Brandts alimtaka Luhende kufanya mazoezi ya pekee wakati wakiendelea na mazoezi hayo kwa kuwa alikuwa hajapona vizuri.
“Bado hajapona vizuri, hivyo hatakiwi mazoezi ya kugongana na wenzake,” alisema Brandts katika mazoezi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kijitonyama jijini Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic