November 27, 2013



Wajumbe wa kamati ya utendaji ya Simba watakutana leo kumjadili kocha mpya waliomtangaza.
 
Kocha mpya aliyetangazwa na Simba ni Zdravko Logarusic raia wa Croatia na aliwahi kuwa kocha wa Gor Mahia ya Kenya.

Wakati wakiwa wamemtangaza kocha mpya, mwenyekiti waliyemsimamisha, Aden Rage alitangaza kuwarejesha Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.

Lakini aliyetangazwa kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Swed Nkwabi amesema suala hilo watalijadili lakini pia watajadili masuala mengine kadhaa.

“Tutakutana na kulijadili suala hilo kwanza kabla ya kutoa mustakabari, hivyo tunaomba mvute subira,” alisema Nkwabi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic