November 5, 2013


Kocha mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ametaka kikosi chake kuendelea kufunga wastani mzuri wa mabao ili kujiwekea akiba.


Brandts raia wa Uholanzi amesema wastani mzuri wa mabao huwa na faida kubwa hasa linapofikia suala la kuwania ubingwa.

“Mabao ni kitu muhimu sana, kama unapata pointi basi ni vziuri kupata mabao mengi.

“Utaona katika mechi kama nne hivi tumekuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao.
“Angalau matatu kila mechi, huu ni mwendo mzuri ambao nimeusisitiza zaidi kwa wachezaji.

“Utaona umuhimu wa mabao mnapofikia mwisho wa ligi, nimezungumza na wachezaji wangu na kuwaeleza hili,” alisema Brandts.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic