November 18, 2013


Aliyekuwa Kocha wa Azam FC, Stewart Hall, tayari ameshaanza kazi yake rasmi katika mradi wa soka chini ya kampuni ya kuzalisha umeme ya Symbion, lakini ametakiwa kuondoka haraka nchini kurudi Uingereza.


Stewart amesema leo mchana ataondoka na kurudi Uingereza ambapo anatakiwa kwenda kuzungumza na uongozi wa Sunderland ambao ndiyo ulioingia mkataba na Kampuni ya Symbion katika kuanzisha mradi huo wa soka nchini.

Stewart amesema mara baada ya kumaliza mazungumzo hayo na uongozi wa Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu England, atarudi Tanzania lakini ataondoka tena kuelekea Nigeria kuangalia kinachoendelea katika mradi kama huo kabla ya kurejea kuendelea na jukumu la kusaka makocha watakaofanya kazi katika kituo hicho.

“Kuna mazungumzo natakiwa kwenda kuzungumza na uongozi wa Sunderland, naondoka hapa kesho (leo) mchana lakini nitarudi hapa baada ya muda mfupi, ingawa nitatakiwa kuondoka tena kuelekea Nigeria, kuna vitu natakiwa kwenda kuangalia kwenye mradi kama huu uliopo huko,” alisema Stewart na kuongeza:


“Nitakaporudi hapa nitaanza na jukumu la kusaka makocha ambao watafanya kazi kwenye mradi, nitatoa mafunzo maalum na makocha ambao watapata nafasi ni wale ambao wana leseni za ukocha.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic