November 26, 2013




Kuonyesha kuwa mazoezi hayana mchezo, wachezaji wa Yanga wamekuwa wakicheza kwa nguvu sana.

Mshambuliaji wa Yanga, Hussein Javu alinusurika kuumia baada ya kiatu cha Nizar Khalfan kumjeruhi kwenye paja.
 

Kutokana na Nizar kuruka na mguu wake kutua kwenye paja lake, Javu alitumia kama dakika nzima akijikagua na akashindwa kuendelea hadi alipopewa matibabu.

Hata hivyo, baadaye Nizar alionekana akimuomba Javu msamaha na kumueleza kuwa ilikuwa ni bahati mbaya.

Chini ya Ernie Brandts, Yanga wamefanya mazoezi leo kwenye Uwanja wa Bora jijini Dar es Salaam kujiandaa na Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili utakaoanza Januari, mwakani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic