November 26, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ametaka wachezaji wote wasiokuwa kwenye vikosi vya timu ya taifa wajiunge na timu yake mazoezini.
 
Brandts amewataka wachezaji ambao hawajaonkana mazoezini kufika mara moja.

“Kila mchezaji ambaye hajaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa anatakiwa mara moja kufika mazoezini na kuungana na wenzake.

“Napenda kuona utaratibu wa  mazoezi unafuatwa na kila mchezaji afike mara moja,” alisema Brandts akiwaeleza baadhi ya maofisa wa benchi la ufundi mara baada ya Yanga kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama, leo.

Baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa wametokea mazoezini ni Mbuyu Twite na Didier Kavumbagu ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic