Klabu ya Simba
inahitajika kumlipa Abdallah Kibadeni shilingi milioni 18 kutokana na kuvunja
mkataba wake wa kuinoa timu hiyo, imefahamika.
Jumanne ya wiki hii Simba ilitangaza
kumtimua kocha huyo pamoja na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambapo nafasi
zao zimechukuliwa na Zdravok Logarusic raia wa Croatia na Seleman Matola.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo
zinaeleza kuwa Kibadeni ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa Sh milioni tatu kwa
mwezi, alikuwa amebakisha mkataba wa miezi sita, hivyo kwa kuwa Simba imeuvunja
mkataba wake, itatakiwa imlipe kiasi cha Sh milioni 18 ambacho ni malipo ya
miezi sita.
“Baada ya mkataba wake kuvunjwa,
Kibadeni anatakiwa kulipwa shilingi milioni kumi na nane, maana alikuwa
analipwa milioni tatu kwa mwezi na alikuwa amebakisha miezi sita katika mkataba
wake,” kilisema chanzo.
Gazeti hili lilipomuuliza Kibadeni juu
ya suala hilo, alisema: “Nasubiri barua yao ya kiofisi ya kuvunja mkataba kisha
ndiyo nitajua juu ya haki yangu ya malipo,” alisema Kibadeni.
SOURCE: CHAMPIONI







0 COMMENTS:
Post a Comment