Katika kuhakikisha nidhamu ya timu
inaongezeka, uongozi wa Mbeya City umeweka sheria ya wachezaji kutonyoa staili
ya kiduku kwenye timu yao.
Kocha mkuu wa Mbeya City, Juma
Mwambusi, alisema huo ni mpango wa kinidhamu ambao viongozi wao wameuweka kuhakikisha
nidhamu inapewa kipaumbele.
Mwambusi alisema mchezaji yeyote
atakayeenda kinyume cha maadili basi hataruhusiwa kuendelea na timu yao, lengo
ni kutimiza malengo yao waliyojiwekea ikiwemo kumaliza Ligi Kuu Bara wakiwa
katika nafasi nzuri.
“Uongozi na timu kwa jumla tuna
malengo yetu tuliyojiwekea mara baada ya kupanda daraja, tunataka kufika mbali
kwenye msimu huu wa ligi kuu na kutokana mikakati tuliyoiweka ninaamini
tutafanikiwa.
“Tumeanza kutengeneza nidhamu kwenye
timu kwa kuwapiga marufuku wachezaji wetu kunyoa kiduku na mitindo mingine yote
ya nywele. Huo ni utaratibu tulioupanga,
ni vema ikatambulika hivyo,” alisema Mwambusi.
0 COMMENTS:
Post a Comment